S. Leone na Ivory Coast Kuchuana

Haki miliki ya picha AP
Image caption Didier Drogba ni mmoja ya wachezaji wa Ivory Coast wanaotarajiwa kushiriki katika mechi dhidi ya Sierra Leone.

Mataifa ya Sierra Leone na Ivory Coast yatawania kufuzu katika mechi za dimba la Afrika watakapokutana usiku wa ijumaa.

Pia siku ya ijumaa, Botswana ni mwenyeji wa Tunisia huku mechi 12 zilizosalia zikigaragazwa siku ya jumamosi.

Ilitangazwa siku ya ijumaa kuwa michuano hiyo itachezwa nchini Equitorial Guinea ambayo imechukua mahala pa Morocco.

Timu ya Ivory Coast inatarajiwa kuimarisha kampeni yake ya kufuzu katika dimba hilo katika kundi Da kupitia kuishinda Sierra Leone mjini Abidjan baada ya kuifunga timu hiyo 2-1 mnamo mwezi Septemba.

Mechi hiyo itachezwa mjini Abidjan kutokana na kuenea kwa ugonjwa hatari wa ebola nchini Sierra Leone.

Ivory Coast ilicharazwa 4-3 na timu ya DRC Congo katika mechi yao ya awali.