Federer ajitoa michuano ya dunia ATP

Haki miliki ya picha AP
Image caption Roger Federer awaaga wapenzi wa mchezo wa Tennis

Mbabe wa Tenis Roger Federer amejiondoa kwenye Fainali ya michuano ya dunia ya ATP ambapo alikua anatarajiwa kuchuana na Novak Djokovic. imeelezwa kuwa chanzo cha kujitoa ni maumivu ya mgongo aliyokua akiyapata....

Mswiss huyo alijitokeza hadharani kwenye uwanja wa 02 Arena mwenyewe na kutangaza kuwa hayuko tayari kucheza .

Federer alimshinda Stan Wawrinka kwa 4-6 7-5 7-6(8-6) siku ya jumamosi katika mchezo wa kusisimua wa nusu fainali ambao ulichezwa kwa saa mbili na dakika 48.