Arsenal yalazwa huku Mancity ikiponea

Image caption Arsenal

Louis Van Gaal alipata ushindi wake wa kwanza ugenini kama meneja wa Manchester United baada ya kuwashinda wapinzani wao wa jadi Arsenal na hivyobasi kupanda hadi nafasi ya nne katika jedwali la ligi ya EPL.

Baada ya kuonyesha mchezo mzuri kwa kipindi kirefu,Kiaran Gibbs alijifunga kufuatia krosi nzuri katika lango la Arsenal iliopigwa na Antonia Valencia kabla ya Wayne Rooney kukamilisha mambo na kuwa 2-0.

Olivier Giroud ambaye aliingia katika kipindi cha pili alifunga bao moja ambalo halikuweza kuimarisha matumani ya Arsenal.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wachezaji wa manchester United

Huku Van Gaal akisheherekea ushindi huo ,matokeo hayo yanaiwacha Arsenal ikiwa na alama 17 kutoka mechi 12 walizocheza ikiwa ni alama kidogo kwa kipindi cha miaka 32 katika ligi ya Uingereza.

Hatahivyo mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger alisema kuwa David De Gea ndio aliyekuwa mchezaji bora katika uwanja wa Emirates baada ya kuokoa mashambulizi mengi ya Arsenal.

Katika matokeo mengine Chelsea iliiendelea na uongozi wa ligi hiyo baada ya kuishinda West Bromwich kwa mabao 2-0 baada ya mchezaji mmoja wa Westborom kuonyeshwa kadi nyekundu.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Manchester City

Nayo manchester City ilitoka nyuma na kuifunga Swansea City 2-1 na kuweka pengo kati yao na viongozi wa ligi Chelsea kuwa alama nane pekee.

Manchester City ambayo ni ya tatu katika ligi walifungwa ndani ya dakika 10 baada ya Wilfried Bony kufunga bao safi.

Lakini mabingwa hao wa ligi walishawazisha baada ya Stevan Jovetic kufunga kupiti krosi iliopigwa na Jesus Navas naye Yaya Toure akafunga bao la ushindi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Chelsea

Matokeo mengine ya ligi kuu ya Uingereza:

Everton 2 - 1 West Ham

Leicester 0 - 0 Sunderland

Newcastle 1 - 0 QPR

Stoke 1 - 2 Burnley.