Casillas kuwania tuzo ya kipa bora zaidi

Image caption Casillas amekuwa na mchezo duni na licha ya hilo ameteuliwa kuwania tuzo ya kipa bora zaidi

Kipa wa Real Madrid na Uhispania Iker Casillas ameorodheshwa kwa timu ya Fifa World 2014 XI licha maonyesho yake mabaya kwenye Kombe la Dunia na kucheza michezo12 tu ligi.

Kipa wa Chelsea Thibaut Courtois yuko kwenye orodha hiyo, pamoja na Manuel Neuer wa Bayern Munich,Claudio Bravo wa Barcelona na Gianluigi Buffon wa Juventus.

Lakini kujumuishwa kwa Casillas kumeshangaza, licha yake kuwa katika timu kwa miaka mitano tangu 2008-2012.

Alicheza mechi mbili tu ya ligi ya La Liga msimu wa 2013-14 na mechi 10 zaidi msimu huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa 33, aliyeinua kombe la Ligi ya Mabingwa na Real, alikosa na kusababisha angalau bao moja katika mechi ya Kombe la Dunia waliocheza Uhispania dhidi ya Uholanzi na Chile, na kuwasababisha kama wamiliki kuondoka baada ya hatua ya makundi.

Courtois anaorodheshwa baada ya kuisaidia klabu ya Atletico Madrid ya Hispania kushinda ligi msimu uliopita wakati akiichezea kwa mkopo,aliendelea kuvutia akichezea Belgium katika Kombe la Dunia hadi robo fainali.

Neuer, ambaye alikuwa katika timu ya mwaka 2013, alikuwa katika lango Ujerumani ailiposhinda mashindano Brazil na pia alishinda vikombe viwili na klabu yake.

Mshindi, atakayepigiwa kura na wachezaji 20,000 duniani kote, atatangazwa tarehe 12 Januari katika tuzo la Ballon d'Or . Walioorodheshwa kwenye nafasi nyingine bado hawajatangazwa.