Wachezaji 10 wachaguliwa tuzo za BBC

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Hamilton pia ametajwa katika tuzo za BBC

Wachezaji kumi wamechaguliwa katika kugombea tuzo ya Mwanasoka bora wa BBC Sport Personality kwa mwaka 2014.

Mcheza Golf Rory McIlroy, mwakasoka Gareth Bale, mcheza sarakasi Max Whitlock, Dereva wa magari ya langa langa Formula 1, Lewis Hamilton na mwogeleaji Adam Peaty ni miongoni mwa WAliopendekezwa.

Wengine ni bondia Carl Froch, Charlotte Dujardin, Mwanariadha Jo Pavey na mchezaji wa michezo ya walemavu Kelly Gallagher.