Arsenal yafuzu,Liverpool yatoka sare

Haki miliki ya picha PA
Image caption Yaya Sanogo afunga bao lake la kwanza katika mechi dhidi ya Borussia Dortmund .Arsenal ilishinda kwa mabao 2-0

Yaya Sanogo aliifungia Arsenal bao lake la kwanza walipoizaba kilabu ya Borusia Dortmund na kuhakikisha wamefuzu katika hatua ya muondoano wa michuano ya kombe la kilabu bingwa barani Ulaya.

Mshambuliaji huyo wa miaka 21 alifunga bao hilo baada ya kushiriki katika mechi 19 bila bao lolote alipomaliza pasi kati yake na Santi carzola mda mchache tu baada ya mechi kuanza.

Alexis Sanchez alifanya mambo kuwa 2-0 baada ya mda wa mapumziko alipopachika bao lililowaacha wengi vinywa wazi.

Vilevile mlinda Lango wa Dortmung aliokoa shambulizi la Sanchez mda mchache baadaye, huku shambulizi jengine la kiungo wa kati wa Arsenal Alex Oxlaide Chamberlain likigonga chuma cha goli.

Arsenal kwa mara ya kwanza walionyesha mchezo uliokomaa huku mabeki wake waliolaumiwa kwa msururu wa matokeo mabaya wakijitahidi vilivyo.

Wachezaji hao waliwazuia washambuliaji wa Dortmund akiwemo Pierre Aubemayang ambaye alikuwa moto wa kuotoa mbali wakati timu hizo mbili zilipokutana kwa mechi yao ya kwanza nchini Ujerumani.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kocha wa timu ya liverpool Brendan Rodgers.Liverpool ilipata sare ya 2-2 katika mechi ya ligi ya kufuzu kwa kombe la kilabu bingwa barani Ulaya.

Wakati huohuo Mkufunzi wa timu ya Liverpool Brendan Rodgers amesema kuwa amefurahishwa na hatua ya timu yake kuchukua udhibiti wa hatma yao hadi mechi ya mwisho katika michuano ya kufuzu kwa raundi za muondoano wa ligi ya kilabu bingwa Ulaya.

Timu hiyo ilifungwa bao la pili katika mda wa majeruhi na kilabu ya Bulgaria Ludogorets na kutoka sare ya 2-2 lakini bado watafuzu katika michuano ya raundi ya maondoano iwapo wataifunga timu ya Bacel mwezi Ujao.

Katika matokeo mengine:

Atl Madrid 4 - 0 Olympiakos

Malmö FF 0 - 2 Juventus

FC Basel 0 - 1 Real Madrid

Zenit St P 1 - 0 Benfica

Bayer Levkn 0 - 1 Monaco

Anderlecht 2 - 0 Galatasaray