Mchezaji wa kriketi Philip Hughes afariki

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hughes alikuwa na umri wa miaka 25

Mchezaji wa Kriketi raia wa Australia Phillip Hughes ameaga Dunia.

Mchezaji huyo amefariki siku chache baada ya kupata majeraha alipogongwa kichwani na mpira siku ya Jumanne wiki hili alipokuwa akicheza mjini Syney.

Ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 25. Awali Madaktari walimfanyia upasuaji kwenye ubongo wake lakini hali yake iliendelea kuwa mbaya

Familia yake inasema kuwa imeshtushwa mno na kifo chake.

Waziri mkuu wa Australia Tony Abbott ameelezea masikitiko yake kuhusiana na kifo cha mcheazji huyo mashuhuri mweney umri mdogo.