Gerrard:Hatujazozana na Kocha

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Steven Gerrard na kocha Brenda Rodgers.

Nahodha wa kilabu ya Liverpool Steven Gerad amepinga kuwepo kwa mzozano wowote kati yake na mkufunzi wa timu hiyo Brendan Rodgers baada ya kuwachwa nje katika mechi kati ya Liverpool na Stoke City.

Ilikuwa mara ya kwanza kwa kiungo huyo wa kati kuwachwa nje tangu mwaka mpya wakati alipokuwa na jeraha.

Hatua hiyo ya Rodgers ya kumwacha nje Gerrad inajiri wakati ambapo nahodha huyo alikuwa anasherehekea miaka 16 tangu ajiunge na timu hiyo.

lakini alisema katika Instagram kwamba mazungumzo ya vyombo vya habari ni ya upuuzi na kwamba hakuna mgogoro wowote kati yao.

Rodgers alikiri kwamba hakujuwa iwapo Gerrad alikuwa anasherehekea kujiunga na kilabu hiyo alipomuwacha nje wakati timu hiyo ilipopata ushindi wa 1-0 katika uwanja wa Anfield.