Balotelli:haikua nia kuashiria ubaguzi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mario Balotelli amekuwa akiandamwa na mashabiki wa soka kwa utovu wa nidhamu

Mshambulaji wa Liverpool Mario Balotelli, ameomba radhi kwa kuweka picha yenye kuashiria vitendo vya kibaguzi katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram. Balotelli 24, mwenye matukio mengi ya utukutu, haraka alifuta picha hiyo iliyokuwa kwenye ukurasa wake wa Instagram.

“naomba radhi kwa yoyote aliekwazika. Nilifikiri kuwa ilikua ni ucheshi na sio ubaguzi ,sikujua kama inaweza kuwa na athari”.

Sakata hili la Balotelli limempelekea kocha wa Arsenal Wenger kuzungumza na kusema wachezaji wanapaswa kujichunga kwa kile wanachoweka kwenye mitandao ya kijamii

“Tunaweza kuwachunga na hatari ila hatuwezi kuwachunga wachezaji saa 24 za siku,wanawajibu wa kujichunga na nakuwa makini kwa kile wanachoandika”.

Nyota huyo wa zamani wa Manchester City na Ac Milan atakosa mchezo wa leo wa ligi dhidi ya Leicester City sababu ni majeruhi.