Newcastle kumkosa Krul kwa majuma sita

Haki miliki ya picha AP
Image caption Meneja wa Newcastle Alan Pardew

Timu ya Newcastle itakosa huduma za kipa wake namba moja Tim Krul kwa kipindi cha majuma sita,kutokana na maumivu ya enka aliyoyapata mazoezini.

Meneja Alan Pardew ameeleza Nyota huyo atakosa michezo mitano ya ligi kuu, na anatarajiwa kurejea dimbani katikati ya Mwezi Januari 2015

Newcastle itamtumia mlinda mlango wake wa pili Rob Elliott kuziba pengo la Tim Krul mpaka katikati ya januari ambako inatazamiwa atakua kapona.

Alan Pardew bado pia anawasiwasi na hali ya mlinzi wake mwenye majeruhi Daryl Janmaat aliyeumia kwenye mchezo dhidi ya West Ham katika dimba la Upton Park.

Newcastle itaendelea kuwakosa mshambuliaji Siem de Jong, viungo Ryan Taylor, Rolando Aarons, Mehdi Abeid na mabeki Fabricio

Coloccini and Davide Santon.walioko nje kwa majeruhi huku viungo Moussa Sissoko na Jack Colback wakiendelea kutumikia adhabu zao.