Afya ya Pele yaimarika

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Pele alikua mahututi baada ya kupata matatizo ya Figo

Hali ya afya ya gwiji wa Soka duniani, Pele imemarika baada ya kutoka kwenye hali ya mahututi.

Pele aliyekua mahututi kwa matatizo ya figo anaendelea vizuri na anauwezo wa kutembea mwenyewe kwa sasa.

"Mgonjwa anaendelea vizuri anaweza kutembea mwenyewe kwenye chumba chake alieleza Albert Einster wa klinik anayotibiwa Pele.Gwiji huyo mwenye miaka 74 ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa Madaktari.