Arsenal yamlenga mjerumani Kramer

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kramer anachezea klabu ya Borussia Monchengladbach

Arsenal wako tayari kutoa pauni milion 20 kumsajili kiungo wa timu ya taifa ya ujerumani Christoph Kramer, 23, anayechezea timu ya Borussia Monchengladbach, iwapo watamkosa nyota Sami Khedira wa Real Madrid.

Kocha wa PSG Laurent Blanc, anampango wa kumchukua mshambuliaji Thierry Henry, Kwa kumpa kandarasi ya muda mfupi.

Galatasaray nao wanawania saini mchezaji hiyo wa zamani wa Arsenal.

Liverpool watatoa ofa ya £25 kumpata kipa wa Fiorentina Neto, ili kuwa mbadala wa Simon Mignolet.

Mshambuliaji Lukas Podolski, 29, anaangalia uwezekano wa kuondoka arsenal mwezi januari na kurejea katika timu yake ya zamani FC Koln .

Inter Milan imeungana na Leicester City, Newcastle katika mbio za kumuwania mshambuliaji Luciano Vietto wa Villarreal.

Kiungo wa brazil Paulinho, 26, anatarajia kurejea nchini Brazil katika klabu ya Sao Paulo au Corinthians.

Boss wa Everton Roberto Martinez amekana kuwepo kwa makubaliano ya mkataba wa kumuuza kiungo James McCarthy 24, kwenda kwa washika bunduki wa London Arsenal.