Arsenal,Chelsea na Mancity uwanjani Leo

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Diego Coasta

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Coast hatashiriki katika mechi dhidi ya Totenham leo usiku baada ya kupata kadi ya njano ya tano siku ya jumamosi na huenda mahala pake pakuchukuliwa na Loic Remy ama Didier Drogba.

Beki Nathan Ake ambaye ana jereha la mguu alikosa mechi ya wikendi dhidi ya Sunderland na huenda asichezee mechi ya leo.

Mlinzi wa Totenham Kyle Naughton hatashiriki katika mechi hiyo baada ya kupigwa marufuku.

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Emmanuel Adebayor

Mshambuliaji wa Totenham Emmanuel Adebayor huenda asishiriki katika mechi hiyo baada ya kupatikana na virusi mbali na kuwa na tatizo la mgongo huku Etienne Capoue na Danny Rose wakikabiliwa na majeraha madogo madogo ya mguuni.

Katika mechi nyengine, beki wa kushoto wa kilabu ya Arsenal Nacho Monreal na kiungo wa kati Alex Oxlade Chamberlain huenda wasishiriki katika mechi dhidi ya Southampton baada ya kupata jereha la goti huku Kieran Gibs akiwa na jeraha la kifundo cha mguu.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Alex Oxlaide Chamberlain

Mlinda lango Wojciech Szczesny ana jeraha la kiuno naye Mikel Arteta akiwa na jeraha la paja na bado watasalia kuwa nje.

Kilabu ya Southampton naye itamkosa Morgan Shneiderlin ambaye alipata jereha katika paja lake katika mechi dhidi ya Manchester City.

Hatahivyo mahala pa kiungo huyo wa kati panaweza kuchukuliwa na Kack Cork ambaye amepona ugonjwa aliokuwa nao.

Image caption Mugubi Wanyama

Harry Reed pia anaweza kuitwa ili kuchukua mahala pake.

Katika mechi kati ya Manchester City na Sunderland nahodha Vincent Kompany hatoshiriki kutokana na jeraha huku Eliakim Mangala akihudumia marafuku ya mechi moja .

Hali hiyo itamlazimu Bacary Sagna kucheza safu ya Ulinzi upande wa kushoto huku Dedryk Boyata akianzishwa.