Van Gaal:Ruhsa kutumia pesa atakavyo

Haki miliki ya picha empics
Image caption Luis Van Gaal akimpa maelekezo Wayne Rooney

Mkuu wa manchester united Louis van Gaal, amepewa ruksa ya kutumia pesa bila ukomo katika kusajili wachezaji anawataka ili kuimarisha kikosi chake.

Man united wametumia £150 milioni kwa usajili wa wachezaji sita Ander Herrera, Luke Shaw, Marcos Rojo, Daley Blind, Radamel Falcao,na Angel Di Maria, aliyevunja rekodi ya usajili nchi uingereza kwa ada ya £59 milioni.

Wakiwa katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu man united wanachangamoto ya kushiriki michuano ya klabu bigwa ulaya msimu ujao.

Bodi ina imani zaidi kwa kocha wake wa sasa kurejesha bahati old traffold kuliko kocha aliyetimuliwa David Moyes.

Van gaal amepewa mamlaka ya kuamua hatma ya mabeki Rafael, Phil Jones, Chris Smalling, Jonny Evans kiungo Anderson mshambuliaji Robin van Persie,ambao mikataba yao inakwisha miezi 18 ijayo.

Klabu wanatarajia kuanzisha mazungumzo ya kandarasi ya kipa David De Gea, ambae kandarasi yake inafika kikomo 2016,pia kumpa ofa ya kandarasi mpya kiungo Michael Carrick kuendelea kubaki.