B.Rodgers:Wacheni kumtegemea Gerrard

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption MKufunzi wa Liverpool Brendan Rodgers

Mkufunzi wa Liverpool Brenda Rodgers amewaonya wachezaji wake kwamba hawafai kumtegemea nahodha wa timu hiyo Steven Gerrard kila mechi.

Amesema kuwa wachezaji hao wanafaa kuziba pengo la nahodha huyo bila wasiwasi wakati ambapo hayupo katika timu.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Nahodha wa timu ya Liverpool Steve Gerrard

Mchezaji huyo wa miaka 34 alipumzishwa kwa mara ya pili mfululizo katika mechi ya nyumbani iliokamilika bila kwa bila.

Licha ya kiungo huyo wa kati kuchezeshwa kunako dakika ya 67 hakuweza kubadilisha mambo uwanjani Anfield.

''Hatuwezi kila mara kumtegemea ,haiwezekani kwamba kila mechi yeye ndiye atakayesababisha mchezo mzuri ama mabao'',alisema Rodgers.