Nigeria na USA kukutana katika dimba

Haki miliki ya picha AP
Image caption Timu za wanawake zikiminyana katika dimba la dunia lilopita.

Canada 2015: Nigeria yapangwa na USA katika kundi gumu la Kombe la Dunia Mabingwa wa Africa; Nigeria wamepangwa katika kundi la kifo la Kombe la dunia la wanawake mwaka 2015 Canada.

Nigeria itachuana na mabingwa wa Olimpiki Marekani katika kundi D katika fainali za za kombe la dunia zitakazochezwa kati ya Juni 6 na Julai 5.

Timu hiyo inayojulikana kama "Super Falcons" pia itachuana na Sweden na Australia katika kundi D mjini Winnipeg.

Kwengineko Ivory Coast itacheza machi zake mjini Ottawa, katika kundi B pamoja na Ujerumani , Norway na Thailand.

Cameroon - taifa la tatu la Afrika kushiriki litachuana na Japan, Switzerland na Ecuador mjini Vancouver.

Hivi ndivyo michuano hiyo ilivyopangwa, . 2015 World Cup draw

Group A Canada China New Zealand Netherlands

Group B Germany Ivory Coast Norway Thailand

Group C Japan Switzerland Cameroon Ecuador

Group D USA Australia Sweden Nigeria

Group E Brazil South Korea Spain Costa Rica

Group F France ENGLAND Colombia Mexico