Radamel Falcao, hali si shwari

Haki miliki ya picha PA
Image caption Mshambuliaji wa Manchester United, Radamel Falcao

Mshambuliaji wa Manchester United Radamel Falcao anauwezo wa kucheza kwa dakika 20 tu kwa mujibu wa kocha wake Louis Van Gaal.

Radamel Falcao, 28,ameingia kutokea bechi kwenye michezo mwili ya mwisho ya Man United baada ya kuwa nje kwa muda kutokana na kuwa majeruhi.

Kocha wa timu hiyo ameeleza “namchagua licha ya ukweli kuwa anauwezo wa kucheza dakika 20 tu”.

Falcao, aliyejiunga na Manchester United msimu huu kwa mkopo toka Monaco anatarajia kuendelea kukaa bechi katika mchezo wa leo dhidi ya Southampton, baada ya mshambuliaji Wayne Rooney kurejea kutoka kwenye maumivu ya goti na akitarajiwa kuanza kikosi cha kwanza.

Mshambuliaji huyo amefunga goli moja mpaka hivi sasa katika michezo aliyochezea kwenye ligi kuu ya Uingereza.