R.Madrid, Juventus,liverpool ni leo

Image caption Liverpool kukipiga na FC Basel usiku wa leo

Liverpool wako kwenye uwanja Michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya itaendelea leo usiku kwa michezo nane kupigwa kwenye viwanja tofauti.

wao wa Anfield wakiwa na kazi moja tu ya kuifunga Fc Basel, katika Mechi yao ya mwisho ya kundi B ili kufuzu kuingia raundi ya Mtoano ya kumi 16 bora.

Usiku huu makundi A hadi D ndio yanacheza Mechi zao za mwisho na tayari Timu 11 zimeshafuzu kucheza Raundi ya Mtoano ya Timu 16,na Jumatano ndio Mechi za mwisho za Makundi zitachezwa ambazo zitatoa Timu 5 zilizobakia za kufuzu .

Nafasi hizo 5 zinagombewa na Timu 11 na miongoni mwao zipo Klabu za Manchester City na Liverpool, huku wenzao Chelsea na Arsenal tayari wameshasonga.

KUNDI A

Juventus v Atletico Madrid

Olympiakos v Malmö FF

KUNDI B

Liverpool v FC Basel

Real Madrid v Ludo Razgrad

KUNDI C

Benfica v Bayer Leverkusenn

Monaco v Zenit Saint Petersburg

KUNDI D

Borussia Dortmd v Anderlecht

Galatasaray v Arsenal