Neville akejeli Manchester United

Image caption Garry Neville enzi zake akichezea Manchester United

Mchezaji wa zamani wa Manchester United Gary Neville amesema kuwa mchuano kati ya timu yake ya jadi na Liverpool hapo Jumapili inalinganishwa na mchezo kati ya "Mbwa au Bata na Simba Mwekundu".

Neville, wakati alipokuwa akifanya kazi na Sky Sports alifananisha mchuano huo na mchezo wa baa.

Na pia alisema kuwa Machester United waliponea kushindwa na Southampton kwa kuibuka washindi kwa 2 -1 jumatatu.

"anaweza kusema atakavyo kwani ni mkongwe lakini kama mkongwe inafaa aelewe yale anayosema" Loius Van Gaal alisema "lazima atilie manane yake maanani"

Lakini Neville amekanusha kuwepo kwa mvutano kati yake na Van Gaal

Robin van Persie aliifungia Manchester United mabao yote mawili katika ushindi wao dhidi ya manchester United

Neviile aliulizwa kwenye mtandao wa Twitter kama kuna mvurugano kati yake na Van Gaal na alisema "mvurugano upi? ambao umebuniwa na haupo"

Van Gaal alikiri kwamba timu yake ilikuwa na bahati nasibu kuishinda Southampton kwani pia wameweza kushinda mechi tano mfululizo.

Ushindi huo uliwezesha Manchester United kupanda hadi nafasi ya tatu