Wenger kuwanyamazisha wakosoaji wake

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Arsen Wenger

Meneja wa Asernal Arserne Wenger anataka kuwanyamazisha wakosoaji wake na ushindi dhidi ya Galatasaray baada ya mashibiki kumkemea kwa sababu ya kushindwa na Stoke 3-2

Arsenali wakiwa wa sita kwenye ligi, Wenger alizomewa na mashabiki alipokuwa akipanda treni.

"lazima tustahimili upinzani, mimi ni mtu anayependa kushindana kinachohitajika ni umuhimi wa mechi zijazo" alisema Wenger

Aliongezea kuwa pia "mi kazi pia, huwezi tafuta wa kulaumu, hatuchezi vizuri na kila mtu anahisi hivyo na unaposhindwa unarejea kwa kishindo"

Arsenal, walimaliza misimu tisa ya kutotwaa kikombe kwa kushinda kombe la FA na wanachuana na Galatasaray katika mechi za vikundi hapo Jumanne kuko Instambul na washatwaa nafasi yao ya kumi na sita bora.

Hata hivyo, wameshindwa mara tatu mechi tano zilizopita na kuhatarisha nafasi yao katika nne bora kwenye ligi.

Wenger alilengwa na shutuma baada ya kushindwa na West Brom 1 - 0 iloiyopelekea mashibiki kizindua kibango kilichosema "Arsene asanti kwa makumbusho lakini ni wakati wa kusema kwaheri"