Kosovo yatambuliwa na kamati ya Olimpic

Haki miliki ya picha AP
Image caption viwanja tarajiwa vya Olimpic

Kamati ya Olimpic ya kimataifa imeitambua Kosovo kama mwanachama wake,hii ina maana kwamba jimbo la Serbia linaweza kuingiza timu katika michuano ya Rio mwaka wa 2016.

Kosovo ilijitangazia uhuru wake mwaka 2008 mpaka sasa haijakubalika ama kuthibitishwa na Umoja wa matataifa kuwa mwanachama wake,yakiwemo mataifa makubwa ulimwenguni kama Urusi na China zimegoma kutambua hilo.

Hata hivyo Serbia adui yake katika vita iliyowagawa ya mwaka 1999 yenyewe inang'ang'ania msimamo kuwa si nchi huru,na kuwakubali wanariadha wa Kosovo ni sawa na mzaha michezoni