Neville na Scholes wamkosoa Van Gaal

Haki miliki ya picha PA
Image caption Louis Van Gaal

Kocha wa kilabu ya Manchester United Louis Van Gaal amewaambia wachezaji wa zamani wa kilabu hiyo Gary NevilLe na mwenzake Paul Scholes kwamba hawajui chochote kinachoendelea katika kilabu hiyo.

Van Gaal anaiongoza timu yake katika mechi ya jumapili dhidi ya mabingwa wa zamani wa ligi ya EPL Liverpool huku Neville akisema kuwa Manchester United inalinda lango lake kama kilabu ya walevi naye Scholes akisema kuwa anahofia kwamba wachezaji chipukizi katika eneo la kazkazini mashariki mwa Uingereza huenda wakaelekea katika uwanja mpya wa kilabu ya Manchester City.

Lakini kocha Van Gaal alimjibu Neville wiki iliopita akimuonya kujihadhari na matamshi yake.'

Image caption Garry Neville Kushoto na Paul Scholes kulia

'Alisema Neville ,''Jengo na malazi katika uwanja wa zoezi sio muhimu,kilicho muhimu ni filosofia na wafanyikazi na baadaye unafaa kutafuta vipaji'',Lakini Van Gaal alimjibu akisema kuwa hana muda wa kutofautisha wafanyikazi wa Mancity na vipaji ,lakini anapoona kile walichonacho yeye hufurahi.

Neville alisema baada ya Manchester United kushinda katika mechi dhidi ya Southampton kwamba mechi ya siku ya ijumaa itakuwa sawa na kuangalia mbwa na Bata wakicheza dhidi ya simba mwekundu.