Mancity,Chelsea na Arsenal zawika

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Frank Lampard aliyeipatia Mancity bao lao la pekee dhidi ya leicester City.

Frank Lampard alifunga bao lake la 175 katika ligi ya Uingereza na kuipatia ushindi wa 1-0 timu yake ya Manchester City dhidi ya kilabu inayoshikilia mkia katika jedwali la Ligi hiyo Leicester.

Mchezaji huyo wa zamani wa kilabu ya Chelsea alipokea pasi muruwa kutoka kwa kiungo wa kati wa Mancity Samir Nasri kabla ya kucheka na wavu na kuipata ushindi wa alama tatu timu yake.

Hatahivyo kocha wa Mancity Manuel Pellegrini atazidi kuuguza majeraha ya wachezaji wake wawili Edin Dzeko na Vincent Kompany.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Olivier Goroud aifungia Arsenal bao la kwanza kupitia kichwa.

Wakati huohuo viongozi wa ligi ya EPL Chelsea wameendeleza ushindi wao baada ya kuishinda timu ya Hull City iliocheza na wachezaji kumi.

Hatahivyo ni kadi nyekundi aliyopewa mchezaji wa Hull ndio iliozua utata katika mechi hiyo baada ya mchezaji Fellipe Louis kudaiwa kujiangusha.

Bao la kwanza lilitiwa kimywani na kiungo wa kati Eden Hazard lakini Chelsea ilihakikisha wametia alama zote kibindoni pale Tom Huddlestone alipomuangusha Louis.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Eden Hazard aifungia Mancity bao la kwanza.

Lakini ni Diego Costa aliyefanya mambo kuwa 2-0 baada ya kufunga akiwa karibu lango la wapinzani.

Nayo Arsenal iliweka shida zake nyuma na kusongea karibu na viongozi wanne wa ligi hiyo baada ya kupata ushindi wa rahisi dhidi ya Newcastle.

Olivier Giroud aliifungia Gunners bao la kwanza baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Alexi Sanchez kabla ya Santi carzola kufanya mambo kuwa 2-0.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Southampton

Giroud aliongeza bao la pili kabla ya Ayoze Feroze kuifungia Newcastle bao la kwanza.

Hatahivyo Santi Carzola alifunga bao la pili na la nne kwa upande wa Arsenal kupitia mkwaju wa penalty baada ya Danny Welbeck kuangushwa katika eneo la hatari.

Matokeo mengine:

Burnley 1 - 0 Southampton

Crystal Palace 1 - 1 Stoke

Sunderland 1 - 1 West Ham

West Brom 1 - 0 Aston Villa