Cristiano Ronaldo atwaa tuzo ya BBC.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Cristiano Ronaldo na kidole cha ushindi

Mshambuliaji Cristiano Ronaldo ametwaa tuzo nyingine baada ya kutangazwa kuwa mwanamichezo bora wa mwaka na shirika la utangazaji la BBC.

Ronaldo alishindwa kuhudhuria sherehe za utoaji tuzo hizo zilizofanyika Glasgow Scotland.kwasababu yuko Morocco na klabu yake ya Real Madrid.

Ronaldo anasema, "Nawashukuru BBC, na mashabiki wangu wa zamani wa Uingereza kwa kunichagua mimi,asanteni sana” Ronaldo amefunga magoli 281 kwenye mechi 267 alizochezea Real Madrid.

Mshambuliaji huyo ametwaa tuzo hiyo akiwashinda mcheza tenesi Serena Williams, bondia Floyd Mayweather na Marc Marquez.