Hatufikirii ubingwa:Van gaal

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Louis van gaal

Baada ya ushindi wa jana dhidi ya Liverpool meneja wa Manchester United Louis van Gaal amegoma kujitumbukiza kwenye mjadala kuwa Timu yake Manchester United sasa wamo rasmi kwenye mbio za kuwania ubigwa.

Man United wapo Nafasi ya 3 kwenye msimo wa Ligi wakiwa Pointi 5 nyuma ya Timu ya Pili Man City na Pointi 8 nyuma ya Chelsea vinara wanaongoza ligi kwa .

Van Gaal alikataa kutamka wazi kama wapo kwenye kinyang’anyiro cha mbio za Ubingwa na badala yake kusema “Nimefurahi sana lakini Mechi ijayo, dhidi ya Aston Villa, ndio muhimu. Ni Mechi ya Ugenini na tuna matatizo na Mechi za Ugenini.”

Man United wameshinda michezo 6 sita mfululizo na kurudisha Imani kwa mashabiki wa timu hiyo baada ya kumaliza msimu uliopita nafasi ya saba chini ya utawala wa kocha David Moyes.