Ratiba ya mabingwa:Ulaya yatolewa

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Timu ya Manchester City

Ratiba ya ligi ya mabigwa barani ulaya hatua ya mtoano imetolewa ambapo vigogo 16 wa soka watachuana kuwania ubigwa wa ulaya .

Mabigwa wa ligi ya Uingereza Manchester City, watakua na kibarua kizito kuwakabili Barcelona ,Chelsea watakipiga na miamba wa soka Ufaransa - Paris St-Germain, huku Arsenal watakabilina Monaco.

Shakhtar Donetsk na Bayern Munich

Schalke na Real Madrid

Juventus na Borussia Dortmund

Bayer Leverkusen na Atletico Madrid

Basel na fc Porto

Mechi za raundi ya mtoano timu 16 bora zitachezwa kwa mfumo wa nyumbani na Ugenini kuanzia Februari 17 mwaka 2015 na Washindi wa kila kundi wataanza kukipiga nyumbani kabla ya kuelekea ugenini.