Chelsea uso kwa uso na Derby County

Haki miliki ya picha PA
Image caption Wachezaji wa Chelsea wakiwa mazoezini

Hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la ligi nchini uingereza maarufu kama (Capital One) itaendelea leo kwa Chelsea kuwa ugenini kwenye uwanja wa iPro Stadium kuwakabili Derby County

Katika mchezo wa leo Chelsea watamkosa mlinzi wao Gary Cahil huku kiungo Cesc Fabregas akirudi baada ya kumaliza kutumikia adhabu

Kwa upande wa Derb County watamkosa beki aliyepewa kadi nyekundi kwenye mchezo dhidi ya Middlesbrough.

Mechi nyingine ya robo fainali ni kati ya Sheffield United, inayocheza Ligi Daraja la 1 ikiwaalika Timu ya Ligi Kuu Southampton,mchezo utakao chezwa kwenye dimba la Bramall Lane.

Mchezo mingine ya robo fainali itaendele tena kesho Siku ya Jumatano, kwa majogoo wa jiji Liverpool kuwa Wageni wa vinara wa ligi daraja la kwanza Bournemouth

Mpambano wa mwisho utakua ni kati ya Newcastle United na Tottenham Hotspur, utakaopigwa White Hart Lane.

Washindi wa mechi hizi watatinga moja kwa moja katika hatua ya nusu fainali.