Waliouza mchezo kushitakiwa,Hispania

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ander Herrera

Mwendesha mashitaka kutoka idara ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini Hispania imeiagiza mahakama kumchunguza kocha wa zamani wa klabu ya Real Zaragoza na baadhi ya wachezaji kutokana na tuhuma za kudaiwa kuuza mchezo.

Tuhuma hizo ni katika mchezo wa kufunga wa msimu wa ligi 2011 ambapo Real Zaragoza iliishinda timu Levante.

Upande wa mashitaka unadai kuwa watuhumiwa wanahusishwa na rushwa ya dola million mbili.

Baadhi ya wachezaji wanaotuhumiwa katika kashfa hiyo ni Ander Herrera, ambaye sasa anachezea zamani na captain wa timu ya Atletico Madrid,Gabi na Javier Aguirre.