EVERTON YAWABANJUA QPR

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Timu ya Everton

Klabu ya Everton imekamilisha michezo ya raundi ya 16 kwa kuichapa mabao 3-1 QPR katika mchezo wa ligi nchi uingereza.

Ross Barkley ndie alianza kuwapa everton goli la kwanza dakika ya 33 Kevin Mirallas alifunga goli la pili na Steven Naismith kumaliza kazi kwa kuipa goli la tatu na kuihakikishia ushindi timu yake.

Mshambuliaji Bobby Zamora akitokea bechi aliifungia QPR goli la kufutia machozi dakika ya 80 ya mchezo.

Kwa ushindi huo Everton wamepanda mpaka nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi na kuwapita mahasimu wao Liverpool walioko nafasi ya 11.