Steve Hanse aongeza mkataba

Haki miliki ya picha AP
Image caption Timu ya Rugby New Zealand

Kocha Steve Hansen wa timu ya Rugby ya New Zealand amesaini kandarasi mpya itayomuweka mpaka mwaka 2017.

Mkataba wa Hansen ulikua unafikia ukingoni mwishoni mwaka 2015, baada ya kumalizika kwa michuano kombe la dunia la mchezo wa Rugby.

Hansen mwenye miaka 55 alikua msaidizi wa kocha wa zamani Graham Henry tangu mwaka 2004. Alichukua mikoba rasmi ya kuwa kocha mkuu wa New Zealand mwaka 2011 baada ya kushinda Kombe la Dunia.

Chini ya utawala wa Hansen New zealand wameshinda mara 38 kati ya michezo 42 wakipoteza michezo miwili na kutoka sare miwili.