Thierry Henry astaafu soka

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Thierry Henry

Mshambuliaji wa zamani wa Klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa Thierry Daniel Henry ametangaza kustaafu kucheza soka rasmi.

Nyota huyu alietwaa kombe la dunia mwaka 1998 akiwa na timu ya Ufaransa alijiondoa kwenye klabu yake New York Red Bulls mapema mwezi huu na kukawa na tetesi atachagua kujiunga na klabu nyingine kubwa barani ulaya.

" Napaswa kuwashukuru mashabiki wote, nawashukuru wachezaji wenzangu na watu binafsi wanaohusika na AS Monaco, Juventus, Arsenal FC, FC Barcelona,na New York Red Bulls na pia Timu ya taifa ya Ufaransa waliufanya wakati wangu wa mchezo kuwa Maalumu".

Henry alianza kuwika katika soka la kimataifa akianzia klabu ya Monaco kisha akaelekea Juventus ,kabla ya kutua Arsenal alikocheza kwa mafanikio makubwa.