Chelsea -nusu fainali Capital Cup.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Chelsea wakipasha

Chelsea, wakicheza katika uwanja wa iPro Stadium waliwachabanga timu ya Derby County, Bao 3-1 kwenye Kombe la Ligi maarufu kama Capital One Cup, na kutinga Nusu Fainali.

Eden Hazard, ndie alianza kuipatia Chelsea, goli la kwanza dakika ya 33 kabla ya Filipe Luis, kufunga goli la pili dakika ya 56 huku Andre Schurrle, akihitimisha ushindi kwa goli la dakika ya 82.

Bao la kufutia machozi kwa Derby lilifungwa na Craig Bryson, Dakika ya 71.

Kwenye Mechi nyingine ya Robo Fainali Sheffield United, waliwashangaza Southampton kwa kuwabanjua Bao 1-0.

Bao la ushindi la Sheffield lilifungwa na McNulty, Dakika ya 63. Southampton walibaki 10 baada ya Gardos kupewa Kadi Nyekundu.

Leo Usiku zitachezwa Robo Fainali nyingine mbili ambapo Liverpool, watakuwa Wageni wa Bournemouth.

Huku katika uwanja wa white Hart Lane Tottenham Hotspur watawakaribisha Newcastle United.