Tomas Berdych,apata kocha mpya

Image caption Tomas Berdych,mchezaji wa Tennis

Mcheza soka namba saba duniani Tomas Berdych amwajirii kocha wa zamani wa Andy Murra Dani Vallverdu kwa msimu wa mwaka 2015. Vallverdu,mwenye miaka 28,aliachana na timu ya Murray mwezi uliopita baada ya kuwa kocha kwa kipindi cha miaka mitano.

Berdych, 29, amekuwa akisaka kocha mwingine ambaye amewahi kuwa na mafanikio makubwa.

Awali mcheza tennis huyu anasema alijaribu kumpata Ivan Lendl,ambaye pia ni mmoja waliomsaidia Murraykufikia malengo lakini ilishindikana kutokana na kutingwa na kazi nyingi.

Murray kwa mara ya kwanza alikutana na Vallverdu wakati wakiwa bado wadogo katika shule ya michezo cha Sanchez-Casal Academy cha nchini Hispania Spain.