Marekani kuandaa olimpiki na Paralympic 2024

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption wanamichezo wa Olimpic

Kamati ya olimpiki nchini Marekani inafanya jitihada za kuandaa michezo Olimpiki na ya mwaka 2024.

Boston, Los Angeles, San Francisco na Washington DC. Mmoja kati ya miji hii utachaguliwa kuwa wenyeji wa michezo hiyo ya olimpiki.

Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya kuwa mwenyeji wa olimpiki kwa kamati ya kimataifa ya Olimpiki (IOC)ni tarehe 15 septemba mwaka 2015,na maamuzi nani atakua mwenyeji yatatolewa mwaka 2017.

Mara ya mwisho kwa Marekani kuandaa michezo Olimpiki kwa majira ya joto ilikua mwaka 1996.

"Kizazi chote cha Wamarekani hakijawahi kuwa na fursa ya kushuhudia tamasha ajabu la Michezo ya Olimpiki na Paralympic katika ardhi ya nyumbani," alisema Mkurugenzi Mtendaji Scott Blackmun.

"Tunaamini ni muhimu kuleta Michezo hii marekani kuhakikisha nguvu ya kudumu ya harakati".

Marekani ni nchi ya tatu baada ya Ujerumani na Italia kuzindua rasmi mchakato wa zabuni wa kuwania kuwa wenyeji wa michezo hiyo.