Drummond miaka minane kutoshiriki riadha

Haki miliki ya picha Getty
Image caption kumekuwa na wimbi la wanamichezo kutumia dawa za kusisimua misuli

Jonh Drummond, ambaye ni mkufunzi wa zamani wa mkimbiaji wa mbio fupi wa Marekani, Tyson Gay, amepigwa marufuku ya miaka minane kwa kosa la kupatikana na matumizi ya dawa za kusisimua misuli.

Kufungiwa kwa mwanariadha huyo kunaanza rasmi leo desemba 17 siku ambayo ni ya kutolewa kwa hukumu hiyo.

Mapema mwaka huu mmarekani huyo aliyewahi kuwa mshindi wa mbio za mita 100 na 200 katika champion ya dunia.

Kwa adhabu hiyo sasa Drummond hatakiwi kujishirikisha kwa namna yoyote katika ufundishaji wa mchezo huo.