Ni Liverpool na Chelsea Capital Cup

Haki miliki ya picha
Image caption Wachezaji wa Liverpool.

Liverpool wakicheza ugenini wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Bournemouth katika michuano ya kombe la Capital Cup.

Majogoo hao wa jiji la london walipata magoli yao kupitia kwa kwa winga Raheem Sterling na Lazar Markovic akihitimisha ushindi uliompa faraja kocha Brendan Rodgers. Bao la kufutia machozi kwa Bournemouth lilifugwa na kiungo Dan Gosling.

Huku katika mchezo mwingine wa robo fainali uliochezwa kwenye uwanja wa White Hart Lane Tottenham waliwachapa Newcastle kwa goli 4­-O,Kwa magoli ya Bentaleb, Chadli, Kane na mshambuliaji Soldado.

Baada ya michezo ya robo fainali kukamilika ratiba ya michezo ys nusu fainali ilijulikana kwa vigogo Chelsea kuchuana na Liverpool huku Tottenham wakiwakabili Sheffield United.