Dan kustaafu baada ya kombe la dunia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bendera ya timu ya New Zealand

Dan Carter Mchezaji wa timu ya taifa ya rugby ya New Zealand atastaafu kuichezea timu ya taifa baada ya kumalizika kwa michezo ya kombe la dunia ya mwaka 2015 itakayofanyika nchini Uingereza.

Carter mwenye miaka 32 atajiunga na timu ya Racing Metro ya Ufaransa na amesaini mkataba wa miaka mitatu.

Kujiunga na timu ya Racing Metro kunamfanya Carter kuwa mcheza Rugby anayelipwa zaidi duniani.

Mchezaji huyo alienza kuichezea timu ya taifa mwaka 2003 ameshinda michezo 102 na kufunga jumla ya pointi 1,457.

Steve Tew Mtendaji mkuu wa rugby New zealand alisema"Nina uhakika mashabiki wa rugby na wa Dan Carter wanasherehekea, amekua mwaminifu nasisi kwa miaka mingi hatuna cha zaidi ya kumshukuru".