Wenger aiogopa Liverpool kufuatia kipigo

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Kocha wa Arsenal Arsene Wenger asema kuwa anaogopa kichapo cha mabao 5-1 dhidi ya timu yake wakati wa mechi kati ya LIverpool na Arsenal msimu uliopita

Kocha wa kilabu ya Arsenal Arsene Wenger amekiri kwamba anaogopa kichapo cha 5-1 alichokipata wakati timu yake ilipochuana na Liverpool msimu uliopita, lakini akaongeza kuwa hatarajii kichapo kama hicho wakati timu hizo mbili zitakapokutana siku ya jumapili.

Arsenal ilikuwa imefungwa mabao 4-0 kufikia dakika ya 20 wakati wa mechi hiyo iliochezwa Anfield huku Liverpool ikiongozwa na mshambuliaji hatari ambaye ameihama kilabu hiyo Luis Suarez.Mechi hiyo ilikamilika ikiwa 5-1 dhidi ya Arsenal.

Lakini meneja huyo wa Arsenal anaamini mengi yamebadilika katika kipindi cha miezi 10,ikiwemo kuondoka kwa Suarez na jeraha la mshambuliaji Daniel Sturridge na mafanikio yake ya kumsajili Alexis Sanchez kutoka Barcelona mbele ya Breanda Rodgers.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Liverpool washerehekea ushindi wao wa 5-0 dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Anfield msimu uliopita.

Wenger alisema;Liverpool ilifunga zaidi ya mabao 100 mwaka uliopita.

Walikuwa wazuri sana katika safu ya mashambulizi,lakini msimu huu wamefunga mabao 19 pekee,hawana tena moto wa kufunga mabao waliokuwa nao.

Walianza kwa mori siku hiyo na sisi tulishindwa kujibu mashambulizi yao.

Kila mechi unayoshindwa inakua kovu katika moyo milele.Lakini tuna kumbukumbu nzuri katika uwanja wa liverpool.

Tulishinda mechi nyingi sana katika uwanja huo,lakini utakumbuka kwamba juma moja baadaye tuliweza kuishinda timu hiyo hiyo tulipocheza nayo nyumbani katika kombe la FA.'