Mancity yapanda kileleni mwa ligi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption David Silva akisherehekea mabao yake mawili dhidi ya Crystal palace.

Kiungo wa kati wa Manchester City David Silva alifunga mabao mawili dhidi ya Crystal Palace na kuiwezesha Manchester City kupanda hadi kilele cha ligi ikiwa sawa na Chelsea.

Mabingwa hao wa Ligi walihangaika kuivunja safu ya ulinzi ya Crystal Palace hadi pale raia huyo wa Uhispania alipopata bao la kwanza katika kipindi cha pili.

Bao lake lililoguswa na mlinzi Scott Dann katika eneo la hatari halikuweza kuokolewa na kipa Speroni.

Baadaye Silva alipata bao lake la pili kutoka krosi iliopigwa na Kolarov kabla ya Yaya Toure kufunga bao lake la tatu baada ya gonga gonga .