Ligi ya soka Somali yaanza

Image caption Msimu wa ligi ya somali waanza Mogadishu

Msimu wa soka nchini Somali umeanza rasmi katika mji mkuu Mogadishu, huku mechi ya kwanza ikichezwa katika uwanja ambao ulikuwa eneo la mazoezi la wapiganaji wa kundi la Alshabaab.

Image caption Msimu wa ligi ya soka Somali waanza

Wanaume,wanawake,wavulana kwa wasichana walifika katika uwanja huo kuona mechi hiyo kati Elman na Horseed ambapo Elman iliibuka kidedea kwa mabao 3-2.