V. Gaal:Bado sifurahishwi na mchezo wetu

Haki miliki ya picha PA
Image caption Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal asema hafurahishwi na mchezo wa kikosi chake

Kocha wa Manchester united Louis Van Gaal amemwambia aliyekuwa kocha wa timu hiyo Alex Furguson kwamba bado hajafurahishwa na mchezo wa kilabu hiyo licha ya kuwa katika nafasi ya tatu katika jedwali la ligi.

Van Gaal hatahivyo anamtarajia kiungo wa kati Angel Dimaria kushiriki katika mechi ya leo kati ya kilabu hiyo na Aston Villa .

Dimaria amekuwa akiuguza jereha la mguu.

Licha ya kwenda Aston Villa na ushindi wa mechi sita mfululizo ,van Gaal anasema kuwa bado anatarajia mchezo mzuri kutoka kwa kikosi chake.

''Wakati ninapoongea na Furguson yye huniambia hakuna shinda umeshinda lakini mimi siangalii mabao pekee ingawaje ndio kiungo muhimu muhimu katika mecho yoyote''.alisena Van Gaal.