Borussia Dortmund yatishiwa kushushwa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption KIlabu ya Borussia Drtmund nchini Ujerumani yahofia kushushwa daraja katika ligi hiyo kutokana na matokeo mabaya msimu huu.

Matokeo mabaya ya kilabu ya ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani Borussia Dortmund yalichukua mwelekeo mpya baada ya kilabu hiyo kushuka na kuorodheshwa miongoni mwa timu ambazo huenda zikateremshwa katika ligi hiyo.

Timu hiyo imeshindwa kwa mara ya 10 baada ya mechi 17 msimu huu na hivyobasi kuwa ya pili kutoka mkiani mwa ligi ya Ujerumani.

Mshambuliaji wa timu ya Warder Bremen Davie Selke na kiungo wa kati Fins Bartel walifunga bao kila mmoja yaliohakikisha kuwa Borussi aDortmund inashuka hadi nafasi ya 17 kati ya timu 18.

Mlinzi wa Ujerumani Matts Hummels aliipatia Dortmund matumaini baada ya kufunga na kichwa.

Licha ya kudhibiti mchezo kwa asilimia 70,Dortmund ilishindwa kuona lango la Bremen.