Liverpool yaapa kuicharaza Arsenal

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kocha wa liverpool Brendan Rodgers

Mshambuliaji wa Liverpool Mario Baloteli atahudumia marufuku ya siku moja kwa kukiuka sheria za shirikisho la soka nchini Uingereza kuhusu mitandao.

Mlinzi Dejan Lovren hajulikanai iwapo atacheza huku daniel Sturridge na Glen Johnson wakisalia nje.

Upande wa Arsenal Alex Oxlaide Chamberlain ,nacho Monreal na Theo walcot wote huenda washiriki kutokana na majeraha.

Calum Chambers amerudi baada ya kupigwa marufuku ,lakini mchezaji Aaron ramsey huenda asishiriki katika mechi zote za Arsenal msimu huu kutokana na jeraha.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kocha wa Arsenal Arsene wenger

Nahodha wa kilabu ya Liverpool Steven Gerrard amekiri kuwa Manchester United ilikuwa bora ikilinganishwa na Liverpool wakati timu hizo mbili zilipochuana wikendi iliopita lakini anasema kuwa hatokubali kushindwa na Arsenal wikendi hii.

Man United iliicharaza Liverpool 3-1 katika mechi hiyo.

Lakini Gerrard anaamini kwamba motisha uliopatikana katika timu hiyo baada ya kuishinda kilabu ya Bournemouth 3-1 katika mechi ya Kombe la Ligi na hivyobasi kuingia katika semi fainali na chelsea inaiweka timu hiyo katika nafasi nzuri dhidi ya Arsenal siku ya jumapili.