Liverpool yaambulia sare kwa Arsenal

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Liverpool na Arsenal zatoka sare

Liverpool, wakiwa uwanja wa nyumbani Anfield, wamenusurika kupata kichapo toka kwa Arsenal kwa kupata sare ya goli 2-2.

Mshambuliaji Philippe Coutinho alianza kuiandika Liverpool goli la kwanza, kabla ya Mathieu Debuchy hajaisawazishia Arsenal, Olivier Giroud akaongeza bao la pili dakika ya 64.

Beki Martin Skrtel alifunga bao la kusawazisha dakika za nyongeza za kipindi cha pili(90+7) kwa mpira wa kichwa uliomshinda kipa wa Wojciech Szczesny

Mshambulaiji Fabio Borini alitolewa nje baada ya kupewa kadi mbili za njano na kuwafanya liverpool kucheza pungufu.

Katika mchezo mwingine wa Sundeland walipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Newcastle United.

Winga Adam Johnson ameibuka shujaa kwa kufunga goli pekee la ushindi kwa upande wa Sunderland, bao la dakika ya 90.

Katika mchezo huo beki wa Newcastle Steven Taylor alipata majeraha baada ya kupasuka eneo la jicho katika heka heka za kumzuia mshambuliaji Steven Fletcher.