Real Madrid ndio kilabu bingwa duniani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Real Madrid washerehekea ushindi wao wa kombe la kilabu bingwa duniani baada ya kuinyuka kilabu ya marekani kusini San Lorenzo 2-0 katika fainali iliochezwa nchini Morrocco.

Kilabu ya Real Madrid imeshinda taji lao la nne mwaka 2014 baada ya kuwashinda mabingwa wa Marekani Kusini kutoka Argentina San Lorenzo katika fainali la za kilabu bingwa duniani zilizochezwa nchini Morrocco.

Mabingwa hao wa kombe la kilabu bingwa barani ulaya,Copa Del Rey na mabingwa wa Super Cup barani Ulaya walianza kufunga kupitia kichwa cha Sergio Ramos.

Makosa ya mlinda lango wa Lorenzo yaliihakikisha ushindi Real madrid baada ya Gareth Bale kuongeza bao la pili.

Real madrid hawakutatizwa na mabingwa hao wa Marekani kusini na hivyobasi kuongeza rekodi yao ya ushindi katika mecho zote kufikia 22.

Ushindi huo pia ni wa kwanza wa kilabu hiyo Bernabeu.