Alastair Cook kufurahia kriketi tena

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Alastair Cook

Mchezaji kriketi Alastair Cook analenga kuendelea kucheza mchezo huo akiwa na furaha.

Alastair Cook mwenye miaka 29 alivuliwa cheo cha unahodha wa timu ya England na kumkatisha tamaa .“lengo langu la kwanza ni kucheza mchezo wangu wa kriket kwa furaha”.

“Natumaini naweza pata mabao na kufurahia mchezo tena”.

Alastar alianza kuingoza timu yake kuanzia mwaka 2011 akiwa na wastani mzuri wa ufungaji katika kila mchezo.

Alastair ataichezea timu ya uingereza itacheyo michezo yake dhidi ya Australia na Afrika kusini kuanzia januari mwakani.