Muhammad Ali augua homa ya mapafu

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sumbwi la haja,la Muhammadi Ali

Mwanamasumbwi nguli na bingwa mara tatu wa uzani wa heavyweight Muhammad Ali amelazwa hospitalini kwa ugonjwa wa homa ya mapafu .

Ali,anapambana na ugonjwa wa kiharusi kwa miaka kadhaa sasa,inaelezwa kuwa hali ya mzio kwenye mapafu na koo lake anaendelea vyema ameeleza msemaji wa nguli huyo ,Bob Gunnell .

Ali ambaye sasa ana umri wa miaka 72 aligunduliwa kuwa na kiharusi mnamo mwaka 1984,ugonjwa huu ulimkumba miaka mitatu baada ya kustaafu masumbwi .

Kwa mara ya mwisho nguli huyu alionekana hadharani katika sherehe za wazi mjini Louisville anakoishi Muhammad Ali alipokwenda kupokea Humanitarian Awards.