Sterling Mwanasoka bora chipukizi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption raheem Sterling

Mshambuliaji kinda wa Liverpool, Raheem Sterling amekabidhiwa Tuzo ya Mwanasoka bora chipukizi mwaka 2014 na Chama cha soka cha England FA.

Sterling alikabidhiwa tuzo hiyo kabla ya Mechi wa ligi kuu ya England kati ya Liverpool dhidi ya Arsenal wakiwa uwanja wa nyumbani Anfield, ambapo mechi hiyo imemalizika kwa sare ya goli 2-2.

FA imekuwa na utaratibu wa kutoa tuzo ya Mwanasoka bora wa mwaka kwa wachezaji chipukizi wanaofanya vizuri katika mchezo wa soka.