Namshukuru Ferguson kuniamini: Van Gaal

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Louis van Gaal

Meneja wa Manchester United amesema kuamini na bosi wa zamani wa timu hiyo Sir Alex Ferguson kumeifanya kazi yake kuwa nyepesi.

Katika msimu wake wa kwanza akiwa na Man United, Louis van Gaal amefanikiwa kuifikisha timu katika nafasi ya tatu pamoja na kuwa na wachezaji wengi majeruhi kitu ambacho kocha aliyepita alishindwa.

"Natumaini atakua msaada kwetu, ameonyesha Imani na kuniamini mimi hicho ndicho kitu kocha anahitaji"

"Ukiwa meneja wa Manchester United, unahitaji Imani na kupata msaada wa mameneja kama Sir Alex Ferguson.Ameeleza Van Gaal.

Ferguson kwa sasa ni mkurugenzi wa timu baada ya kustaafu kazi ya ukocha.