Katibu mkuu mpya Yanga Jonas Tibohora .

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Nembo ya Club ya Yanga

katibu mkuu mpya wa YANGA Jonas Tibohora ameahidi makubwa kwenye klabu ya Yanga.Dr Jonas Tibohora leo amezungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani.

Jonas anataka kuiongoza Yanga kujiendesha kiuchumi, katika mpango wake huo anataka kuanza kutengeneza kikosi imara cha ushindani ikiwa ni pamoja na kutengeneza mifumo bora ya soka la vijana klabuni hapo.

Lengo kubwa la kuwekeza kwenye timu za vijana ni kujaribu kupunguza gharama za kununua wachezaji kutoka nje,pia amesema sasa ni muda wa klabu hiyo kunufaika na nembo ya klabu hiyo kibiashara.